Mwanaume anapotoka nje ya ndoa, hatoki kwa sababau anataka sana kutoka,
hutoka zaidi kwa sababu kuna msukumo wa kutoka. Hatoki nje kwa sababu
anampenda huyo anayetoka naye nje, hapana. Anatoka nje kwa sababau
anasukumwa na asichokijua.
Kwa nini mwanaume anatoka nje na anafumaniwa, anaomba radhi, anasamehewa
na halafu anatoka tena nje. Mke akitaka kuondoka, anatumia kila gharama
kumzuia. Kama hampendi anamzuia wa kazi gani? Kama ingekuwa kutoka nje
ni sawa na kupenda kwa mwanaume, si angeachana na mkewe na kubaki na
huyo hawara?
Ni kweli kwamba, baadhi ya wanaume hutoka nje kwa sababau wamewachoka
wake zao, lakini wengi hutoka nje kwa kusukumwa na mauambile tu.
Mwanaume huvutwa na mwili tu wa mwanamke, siyo kitu kingine. Kwa namna
anavyovaa tu, mwanamke huweza kumvuta mwanaume kwa kiwango cha juu sana.
Nikisema kumvuta nina maana ya kumtamanisha.
Wataalamu wengi wanasema nguo zenye kuchokoza kama vile zile za kubana
au nusu uchi kwa ujumla, huamsha hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume kwa
kiwango kikubwa zaidi, kuliko mwili wa kike ulio uchi.
Kwa hiyo wanawake wana changamoto kuhakikisha kwamba, wakati mwingine
wasione aibu kuwalinda waume au wapenzi wao, kwani linapokuja suala la
kutamani na kutenda, wanaume zao ni sawa na Beberu la mbuzi. Hadi
wamalize au kukamilisha kiu yao, ndipo akili zao za kibinadamu
zinaporejea.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page