HAYA NDIO MADHAIFU MATANO (5) YANAYODIDIMIZA MAHUSIANO NA NDOA

 
Makalahii ni tafakari huru kuhusu mambo ya msingi katika mahusiano. Hapa utapata tafakari ya maana ya maneno naimani ambazo zinatutatiza wengi wetu. 1. Mchanganyiko mkubwa kuhusu maana yamahusiano, mapenzi na ndoa: Labdakipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini yasiwepomahusiano... wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndioukweli wenyewe. Ndoa ni namna tuu ambayowawili walio kwenye
mahusiano wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa waowapo rasmi katika mahusiano. Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namnaya kutaka kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokeakuvunjika, basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo zandoa husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi, kugawanamali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa unaweka kiapo kwaMungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo unayemchagua. Hivyobasi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi.
Kiuhalisi inabidi kwanza yawepomahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume
cha hivyo nikuwa unakula kiapo 'feki'. Ndiomaana basi, ni muhimu kwa wapenzi kutambua kweli kama wanahitajiana, kuwakwenye mahusiano na kutafakari kwa uhuru kama kweli wanataka kuweka kiapo rasmicha kuwa pamoja. Kutumiandoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni maamuzi magumu ambayopengine yanaweza yasilete faida hapo baadae.

2.Mahusiano na ndoa nyingi huyumbishwa naMatarajio yasiyo halisi Kablahata ya kuingia katika mahusiano na hatimaye ndoa wengi wetu huwa na matarajiobinafsi ya kimaisha. Matarajio haya yanajumuisha vile tunavyotaka sie wenyewekuwa hapo baadae, pamoja na matarajio ya vile tunavyotaka wenza wetu wawe. Hatahivyo katika hali

halisi tunajikuta sisi wenyewe hatuwezi kujibadilisha aukujiweka kwa usahihi vile tunavyotamani kuwa (kwa sababu kwa kila tunachojaribukufanya kuwa bora, tunajikuta bado tuna madhaifu mawili matatu). Pamoja naukweli huu, tunajikuta tupo na matarajio ya kuwafanya wenza wetu wawe watu waaina fulani. Kwakuwa kiasili binadamu ni kiumbe huru, tunajikuta wenza
wetu naowakiwa 'busy' kutimiza ndoto za vile wanavyotamani kuwa iwe kimavazi, aina yamarafiki,
utafutaji wa kazi , kujiendeleza kimasomo, aina ya mali za kununua,hata kufikiria tofauti aina ya maisha wanayotaka muishi. Matokeoyake ukinzani huu wa matarajio ni mkanganyiko wa mgongano wa mawazo kati yawawili nyie, na mwanzo wa vita ya chini kwa chini ya nguvu ya maamuzi katikamahusiano yenu.

3. Kuweza kumbadili tabia mwenza wako Mojawapoya jambo ambalo hufanywa na wengi walio katika mahusiano ni kuwa na 'tamaa' yakutaka kumbadili tabia fulani mwenza wake. Hata hivyo 'tamaa' hii ni sehemu yayale tunayoyaita matarajio yasiyo halisi, kwani tabia ya mtu hujengwa na mambomengi sana, ikijumuisha aina ya makuzi, aina ya mfumo wa imani mtu anaouamini,aina ya marafiki alio nao, uwezo wake wa kujiamini katika kubadili tabia kwaniwengine wameshakata tamaa kuwa hawawezi kukata tamaa, na zaidi sana, mabadilikoya tabia huhitaji mfumo endelevu na wenye kusoma vema asili ya tabia ili kuwezakuirekebisha. Hatahivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea 'mapenzi'au vitisho tuu kama
vile'nitakuacha mie ', kama sababu yakumfanya mtu abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili
ya tabia yamtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya zoezi lakubadilishana tabia kuwa gumu na pengine lisilowezakana.

4. Kuvumilia ndio kuonyesha upendo na ndiokudumisha mahusiano Hiini aina nyingine ya matarajio ambayo sio halisi kwani kiukweli kila mtu analojukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba 'uzembe' wamwingine kwa kisingizio tuu cha kuwa unaonyesha upendo hususani pale ambapo nikwa
uzembe tuu au kutokujali kwake mwenza husika amefanya jambo fulani. Kwajinsi kasumba hii ilivyo enea sio ajabu kukuta mtu akifanya mambo mabaya kwamwenza wake kwa makusudi ili tuu eti apime kama kweli mwenza wake ni mvumilivu. Kumbukahapa hatumaanishi kuwa kusamehe ni kosa. Hapana, kusameheana ni muhimu, lakinisio kwamba ni muhimu tuu katika mapenzi. Kusameheana ni jambo la asili, natunapaswa
kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano.
Tunachosemani kuwa kuna kasumba ya baadhi yetukuona kuwa wanayo 'haki' ya msingi ya kukosea eti tuu kwakuwa tuu mwenza wakeanalazimika kusamehe ili kuonyesha kweli anao upendo wa dhati. Amini usiamini, kasumba hii ya kutarajia ainaya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio
tuu cha kuwa upo kwenyemapenzi namwenza wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwanimwenzi wako nae ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha,isitoshe na yeye anahitaji upendo na
kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia kwakokusamehewa na kuvumiliwa kuna mnyima haki mwenza wako. Hatimaye kutegema kwakokusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie mashaka upendo wakokwake.

5. Uaminifu = Upendo= Kudumu kwa mahusiano Pamojana ukweli kuwa mwenza wako anatarajia utakuwa muanifu kwake, elewa kuwa kuwamwaminifu pekee katika mahusiano yako sio tiketi ya kudumu kwa mahusiano yenukwakuwa watu wanaingia kwenye mahusiano sio tuu kwa kuwa wanataka kuwa na mtummoja muaminifu bali wana mahitaji mengine wanayohitaji. Zungumzana mwenza wako, fanya utafiti wako binafsi kuhusu mpenzi wako ujue mambomengine anayohitaji toka kwako. Pia msikilize anapokutaka urekebishe mambokadhaa au ufanye mambo fulani. Inapendeza pale unapomfanyia mtu
mamboyanayompendezesha kwa kuwa hivyo ndivyo anavyotaka, sio kwakuwa tuu weweunadhani kufanya hivyo kutampendezesha mhusika.
CHANGIA MTAZAMO NA MAONI YAKO JUU YA HII MADA..
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page