Mapenzi
ni kitu Fulani tofauti sana kwenye hii dunia na hata nje ya hii sayari.
Mapenzi kwa kiasi kikubwa sana yanasababisha hata mambo mengine kwenye
hii dunia yaende sawa au yaende tofauti hata kama hayahusiani na
mahusiano ya mapenzi. Vifo vingi hutokana na mapenzi, kuna magonjwa watu
wanaumwa kisa mapenzi, kuna mambo watu wanayafanya si ya kawaida kisa
mapenzi.
Ukiachilia
mbali PESA, Mapenzi huwa yana nafasi kubwa sana kwenye kitu chochote
ndani yahii dunia tunayoishi. Si masikini wala si tajiri, wote kwa
pamoja wanahitaji mapenzi kutoka kwa wanaowapenda ili dunia iweze kwenda
sawa kwa upande wao. Na ndio sababu hata mimi hapa ninaandika kuhusu
mapenzi kwa sababu yananigusa hata mimi na hata wewe unayesoma hapa
sasa.
Ukipata
mpenzi anayekuelewa na kukupenda basi hata dunia iwe ya tabu vipi kwako
utaiona inazunguka kama kawaida na maisha yatasonga mbele kwako kwa
raha mustarehe, na hata matatizo mengine makubwa kwako huwa madogo kwa
sababu tu unapenda na kupendwa kwa dhati.
Lakini
ukiumizwa kwenye mapenzi au kutojaliwa kama wewe unavyojali basi hata
dunia iwe na raha gani kwako utaiona chungu na hata raha ya maisha
hutakuwa nayo hata kama una hela kiasi gani na hata kama una cheo
kikubwa kama mfalme au hata rais. Wengine hufikia hatu ya kuteseka tu
bila kuondoka kwenye mahusiano kwa kuogopa kuumizwa tena huko waendapo
na wengine huondoka baadae sana wakiwa tayari wameshachelewa.
Kuna
Sababu Nyingi Sana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye
mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Mojawapo
kati ya sababu hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;-
1. UONGO.
Hakuna
kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si
mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na
uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama
mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna
vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo
kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko
kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa
matatizo na unaweza kusababisha kuachana.
2. USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni
mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa
kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora
kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu
moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina
mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima
avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.
Kama
kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora
umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa
shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na
kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa
huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza
kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.
3. ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna
kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa
dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi
ya wewe.
Huwa
inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza
kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo.
Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi.
Kamwe
Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako,
Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini
Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya
Mapenzi Ipo, Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli
Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.
4. DHARAU.
Hii
pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza
kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali
yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake
au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
Na
hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana
akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara
nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi
wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa
Hakuna
kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako kukukimbia au hata kukosa
uaminifu na wewe kama akija kugundua kama wewe ni mropokaji na huna
‘’kifua’’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na hayakutakiwa
kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na huwa
inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako then yeye anaenda
kusimulia.
Mambo
mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini kesho unaenda mtaani unakuta
kila mtu anajua mlichofanya tena wanakuhadithia kama walikuwepo vile,
hiyo si kitu nzuri na itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi unayempata.
6. TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa
ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine
kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na mmeamua kupendana kwa
shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na kukosa uvumilivu
hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.
Kama
mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua kuwa naye basi usiwe na tama
kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia mahusiano yako kukosa
nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu kama
unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya
lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi zinazoweza
kuku-cost hapo baadae.
7. KUKOSA MSIMAMO.
Hii
kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi ya siku hizi. Nadhani ni hali
halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na teknolojia tuliyonayo
ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao na vyombo mbali
mbali vya habari.
Wapenzi
wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano yao na
unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na wanakuwa
hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa mpenzi
wake.
8. KUTOJALI/KUTOKUWA NA MSAADA.
Hii
pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana na kupelekea kushuka kwa thamani ya
mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa duniani. Kama kweli unampenda
mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na umjali na kumchukulia
kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia majukumu bila
sababu zote za msingi.
Kama huwezi kujali na kusaidia basi usiingie kwenye mahusiano ni bora ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu usiyotakiwa.
9. UBAHILI.
Huna
sababu yoyote ya kuwa na pesa na mpenzi wako akawa anapata tabu kama
vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa mambo yasiyo na msingi lakini
at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako kila unapohitajika.
Kuna
vitu vingine hata huhitaji kuambiwa kama unatakiwa kuvishughulikia, ni
wewe mwenyewe tu kuwa responsible kumhudumia mpenzi wako. Na hii huwa
ina-apply sana kwa wavulana kutokana na kasumba iliyojengeka na mila
tulizozikuta.
10. USHOGA/USAGAJI
Hii
ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu anayependa mtu wake awe Shoga kama
ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana. Ni aibu kubwa sana kwa
mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani kwa akili ya
kawaida kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama
utakishuhudia kwa macho ya
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page