NAMPENDA DADA YANGU........NAOMBENI MNISAIDIE USHAURI

 

Shikamoo shangazi mkubwa. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27. Nimetokea kumpenda dada yangu mtoto wa mama yangu mdogo. Nafikiri Mungu akipenda nitamuoa huko baadaye. Ila bado sijamwambia
kuhusu hisia zangu. Lakini kabla sijaanza hatua yeyote nilikuwa nataka kujua; Je, itakuwa sawa tukiamua kuoana hasa ukizingatia kuwa sisi ni ndugu? Hii imekaaje katika tamaduni zetu za kitanzania?
Mohamed
Dar
Natumai wewe ni muumini wa dini ya Kiislamu. Ukienda kwenye dini yako hilo siyo tatizo. Lakini linapokuja suala la utamaduni, Kitanzania huwezi kumuoa, kwani huyo ni dada yako.
Mama kaniletea mchumba kutoka kijijini
Shangazi mkubwa mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30. Niliondoka kijijni kwetu huko Uzaramoni muda mrefu. Hivi sasa ninaishi Morogoro nikiwa mfanyakazi serikalini. Nikiwa huku nilitokea kumpenda msichana mmoja ambaye nahisi ndiye atakuwa mke wangu. Nikiwa kwenye taratibu za kuwajulisha wazazi wangu, mama amekuja na kuniletea msichana mwingine kutoka kijijini akitaka nimuoe.
Shangazi, naomba unishauri, nifanye nini?
Gasper
Morogoro
Wala huna haja ya kumung’unya maneno, mweke wazi mama yako, umwambie kuwa tayari umempata atakayekufaa.
Nasumbuliwa na wanafunzi wenzangu wa kike
CHANGIA MTAZAMO NA MAONI YAKO JUU YA HII MADA..
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page