Mimi
ni mwanafunzi wa chuo fulani
hapa nchini Tanzania. Kuna Profesa mmoja wa hapa chuoni kwetu
ameanzisha uhusiano na mpenzi wangu ambaye nilikuwa nampenda sana na
nilitegemea awe mama wa watoto wangu. Pamoja na kwamba nilikuwa nampenda
sana
lakini nililazimika kuachana naye ili kuepuka migogoro ambayo
ingenisababishia
matatizo katika masomo yangu.
Binti yule alilia sana na kunibembeleza nikubali heti kwasababu alikuwa ametumwa na Profesa aniletee mimi. Nilikana kwa herufi kubwa na kumfukuza kama mwizi.
Ilipofika mitihani ya majaribio nikaona performance yangu inashuka na baadhi ya mitihani yangu ikapotea na kuambiwa heti sikufanya test. Hata hivyo somo la yule Profesa nikawa ninafauru vizuri ingawa nilikuwa sijiandai ipasavyo kama masomo mengine. Nimefuatilia sana lakini sikuambulia kitu zaidi ya kuambiwa heti nisubiri kurudia masomo ambayo sikuwa nimeyafanyia test. Nimeumia sana kwasababu nilikuwa mwaka wa mwisho.
Pamoja na kwamba nimeumia sana kurudia mwaka lakini kinachonichanganya zaidi ni kwamba mwalimu yule bado yupo pale chuoni. Sijajua kitu ambacho kinaweza kutokea katika mwaka huu mpya wa masomo ambao sikustahili kuwa chuoni.
JE, NIFANYE NINI ILI KUWEZA KUEPUKANA NA VITIMBI VYA PROFESA HUYU?
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page