Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makaliao
makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.
Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno.
Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka.
Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.ILA IKUMBUKWE MAKALIO NA HIPSI ZINAZOONGELEWA HAPO JUU NI ORIGINAL TU..KWA WALE WALIO YAPATA DUKANI HAPA HAMHUSIKI.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page