Ndugu wana dira la mahusiano nina mchumba ambaye tumedumu kwa miaka miwili,kiundani
nampenda sana ila yeye hanionyeshi mapenzi ya kweli yaani nisipopiga
simu anaweza kukaa kimya hata siku nzima pia hapendi kujishusha na
kukubali makosa yake hata kuomba msamaha ni vigumu mwezi uliopita
nimekutana na msichana mwingine anayenivutia sana(very cute) na anadai
yeye ni bikira ambaye ameweka nadhiri na Mungu kutofanya mapenzi mpaka
ndoa kwa uzoefu wangu kweli inaonyesha hajawahi kuwa na mtu maana aibu
imemjaa usoni na pia kwa umri wake(20yrs) kuna uwezekano anachosema ni
kweli,mimi pia msichana niliyenae ndio wa kwanza napata shida kumkubali
huyu dogo maana niliyenae nampenda sana najisikia hatia kumsaliti na
kumwacha na huyu ndio muda mwingi ananitafuta,kiukweli nipo kwenye njia
panda
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page