JE UTAJUAJE MWANAMKE HUYU ANAKUSALITI..?

 

Kwa wasichana nivyema wote kulichunguza hili ili kutambuwa kama kunaanaye kuibia penzi. Siombaya kuhisi kama kunaanaye taka kukuibia mpenzi maana ni kitu ambacho kipo kwenye mahusiano.
Tazama dalili zifuatazo.
Je inaonekana kama msichana mwingine au rafiki yako anapenda kutembea sana pamoja na mpenzi wako?
Je inaonyesha kama anapenda sana kuzungumza na mpenzi wako?
Hali hii ni yahatari na inaweza kupelekea yeye kumdanganya mpenzi wako na kusababisha kwa wewe kuachika na kuwa na mpenzi wako.
Namana ya kushughulikia tatizo hili, Kama mpo kwenye mahusiano mahususi na mnamipango ya kuishi pamoja ni vyema umwite mpenzio na kumuuliza ninini kinachoendelea na kueleza hisia zako zilizopo juu ya hali inayoendelea kwenye mahusiano yenu.
Kama mpenzi wako ana kupenda kwa dhati basi atafuata uyasemayo, Lakini pia isiishie hapo, Unaweza kufuatilia pia mwenendo wa mahusiano ya mwizi wako kwa mpenzi wako na kujaribu kutambuwa kama bado anamnyemelea uweze kuokoa penzi lako.
Tazama kama wanatazamana:
Nivyema kuchunguza ishara za macho, nakujaribu kuiba kwa macho ili ujue kama penzi lako lipo au linaibiwa na rafiki yako. Na ikiwezekana unaweza kumuuliza na kumuonya inapobidi.
Chunguza kinachotokea kwenye hali fulani:
Mfano wakati ukiwa unarudi au umewakuta pamoja, Je yule mwizi wako atashtuka, atachukia au ataondoka? Hii inamaanisha hayupo anawasiwasi wa kuweza kufumaniwa au kugunduliwa kwa tabia yake ya uizi wa penzi.
Angalia kuwa na wivu na hali ya hatari:
Je mwizi wako anachukuliaje pale unapokuwa na mpenzi wako, Anaonyesha wivu au hali gani? Nidhahiri akionyesha wivu atakuwa sio mwema wa penzi lako.
Hakikisha Unavaa vizuri:
Ili umshinde mwizi wa penzi lako hakikisha una vyaa vyema na kujiweka msafi kuhakikisha hauatarishi penzi lako na kupelekea kuachika kwa ushindani wa mwizi wa penzi.
Sikuzote kwenye mapenzi usikubali kumuacha mpenzi wako akachukuliwa na mwingine, Wasichana wengi wamekuwa mwakiona ushindani ni mkubwa basi wanaachia penzi na kuliacha lipotee. Usifanye hivyo kwani itakuumiza na kukuvunja moto.
CHANGIA MTAZAMO NA MAONI YAKO JUU YA HII MADA..
Facebook Comments Plugin Enhanced by Dira la mahusiano FB page