Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa!
Hakuna
kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana
lakini huwa anadai hakuna tatizo! Najiuliza sana hivi kutoka nje ya ndoa
kutanosaidia nini? Nitachinwa pesa bure na ndo matatizo yataongezeka
lakini pia kiimani hairuhusiwi nami naogopa kukutwa katika dhambi na
Mungu wangu!
Nimesali
sana lakini kama hakuna badiliko lolote! Nimuache? Yaani kila kitu tabu
tupu! Wasichana nawaogopa mno nahisi wataniongeza machungu je,
nitamfute mmama wa wastani kama miaka 34 ila awe mzuri? mi nina 25.
Kwakweli sijitambui niko njia panda!
Nilikuwa mwajiriwa wa
kampuni fulani na nilikuwa nikilipwa laki 5 kwa mwezi sasa nina miezi 2
nkmeacha kazi sababu ya matatizo ya ndoa yangu!
Sijielewi nahisi
naelekea kufa ningepata mwanamke wa umri huo na anaishi tofauti na.mji
wangu na akanipenda ningeenda kukaa kwake hata kwa miezi 3.
Nahisi maisha yangu yanaharibika sasa,
Nina
uchungu sana usiku huu nilikuwa safari nimerudi na zawadi zimepokelewa
na kutupwa sitting rum, ninahamu nimemsogelea kitandani kanipiga pepisi
jichoni nomeumia sana maana tangu tuoane sijawahi ifurahia ndoa!
Hapa
najiuliza nifanyeje napanga nitoke nikalale guest lakini sina hata
wakunifariji natoka naenda guest hata nikifika nikaamua kujitoa duniani
inatosha.
Kuna wanawake wazuri sana, wapoleee sauti za upole
akikukosea kidogo tu utasikia samahani baba yangu, nakupenda haikuwa nia
yangu, jaman namimi si nipate mmoja wa hivi?