Makalahii ni tafakari huru kuhusu mambo ya msingi katika mahusiano. Hapa utapata tafakari ya maana
ya maneno naimani ambazo zinatutatiza wengi wetu.
1.
Mchanganyiko mkubwa kuhusu maana yamahusiano, mapenzi na ndoa:
Labdakipengele hiki tuanze kwa kueleza kuwa kunaweza kuwepo ndoa, lakini
yasiwepomahusiano... wala mapenzi. Inaweza kuonekana kama inachanganya kidogo, lakini ndioukweli wenyewe. Ndoa ni namna tuu ambayowawili walio kwenye
mahusiano
wanaamua kuwataarifu rasmi watu wengine kuwa waowapo rasmi katika
mahusiano. Ndoa ni kiapo mbele ya watu wengine , na ni namnaya kutaka
kumuhakikishia mwenza wako kuwa endapo kiapo hicho kitatokeakuvunjika,
basi unakubali rasmi kuwajibika kwa mujibu wa taratibu zilizopo zandoa
husika, ikiwemo kukubali kuitwa kwenye mabaraza ya usuluhishi,
kugawanamali, n.k. Na kwa upande wa kiroho, inabeba maana zaidi kuwa
unaweka kiapo kwaMungu wako kuwa utalinda mahusiano yako na huyo
unayemchagua. Hivyobasi, ndoa haijengi mahusiano wala mapenzi.
Kiuhalisi inabidi kwanza yawepomahusiano na mapenzi kisha ndio kiapo kifanyike, kwani kinyume
cha
hivyo nikuwa unakula kiapo 'feki'. Ndiomaana basi, ni muhimu kwa
wapenzi kutambua kweli kama wanahitajiana, kuwakwenye mahusiano na
kutafakari kwa uhuru kama kweli wanataka kuweka kiapo rasmicha kuwa
pamoja. Kutumiandoa kama kinga ya kuhakikisha mahusiano yako yanadumu ni
maamuzi magumu ambayopengine yanaweza yasilete faida hapo baadae.
2.Mahusiano
na ndoa nyingi huyumbishwa naMatarajio yasiyo halisi Kablahata ya
kuingia katika mahusiano na hatimaye ndoa wengi wetu huwa na
matarajiobinafsi ya kimaisha. Matarajio haya yanajumuisha vile
tunavyotaka sie wenyewekuwa hapo baadae, pamoja na matarajio ya vile
tunavyotaka wenza wetu wawe. Hatahivyo katika hali
halisi
tunajikuta sisi wenyewe hatuwezi kujibadilisha aukujiweka kwa usahihi
vile tunavyotamani kuwa (kwa sababu kwa kila tunachojaribukufanya kuwa
bora, tunajikuta bado tuna madhaifu mawili matatu). Pamoja naukweli huu,
tunajikuta tupo na matarajio ya kuwafanya wenza wetu wawe watu waaina
fulani. Kwakuwa kiasili binadamu ni kiumbe huru, tunajikuta wenza
wetu naowakiwa 'busy' kutimiza ndoto za vile wanavyotamani kuwa iwe kimavazi, aina yamarafiki,
utafutaji
wa kazi , kujiendeleza kimasomo, aina ya mali za kununua,hata kufikiria
tofauti aina ya maisha wanayotaka muishi. Matokeoyake ukinzani huu wa
matarajio ni mkanganyiko wa mgongano wa mawazo kati yawawili nyie, na
mwanzo wa vita ya chini kwa chini ya nguvu ya maamuzi katikamahusiano
yenu.
3. Kuweza kumbadili tabia mwenza wako Mojawapoya jambo
ambalo hufanywa na wengi walio katika mahusiano ni kuwa na 'tamaa'
yakutaka kumbadili tabia fulani mwenza wake. Hata hivyo 'tamaa' hii ni
sehemu yayale tunayoyaita matarajio yasiyo halisi, kwani tabia ya mtu
hujengwa na mambomengi sana, ikijumuisha aina ya makuzi, aina ya mfumo
wa imani mtu anaouamini,aina ya marafiki alio nao, uwezo wake wa
kujiamini katika kubadili tabia kwaniwengine wameshakata tamaa kuwa
hawawezi kukata tamaa, na zaidi sana, mabadilikoya tabia huhitaji mfumo
endelevu na wenye kusoma vema asili ya tabia ili kuwezakuirekebisha.
Hatahivyo wengi wetu kwenye mahusiano, hutegemea 'mapenzi'au vitisho tuu
kama
vile'nitakuacha mie ', kama sababu yakumfanya mtu abadilike kitabia.Udhaifu wetu katika kutambua asili
ya
tabia yamtu husika na mbinu za kisayansi za kubadili tabia hufanya
zoezi lakubadilishana tabia kuwa gumu na pengine lisilowezakana.
4.
Kuvumilia ndio kuonyesha upendo na ndiokudumisha mahusiano Hiini aina
nyingine ya matarajio ambayo sio halisi kwani kiukweli kila mtu
analojukumu la kufanya bidii kuwa mtu mwema, hivyo hauhitaji kubeba
'uzembe' wamwingine kwa kisingizio tuu cha kuwa unaonyesha upendo
hususani pale ambapo nikwa
uzembe tuu au kutokujali kwake mwenza
husika amefanya jambo fulani. Kwajinsi kasumba hii ilivyo enea sio ajabu
kukuta mtu akifanya mambo mabaya kwamwenza wake kwa makusudi ili tuu
eti apime kama kweli mwenza wake ni mvumilivu. Kumbukahapa hatumaanishi
kuwa kusamehe ni kosa. Hapana, kusameheana ni muhimu, lakinisio kwamba
ni muhimu tuu katika mapenzi. Kusameheana ni jambo la asili, natunapaswa
kusameheana kwa mambo mengi nje hata ya mahusiano.
Tunachosemani
kuwa kuna kasumba ya baadhi yetukuona kuwa wanayo 'haki' ya msingi ya
kukosea eti tuu kwakuwa tuu mwenza wakeanalazimika kusamehe ili
kuonyesha kweli anao upendo wa dhati. Amini usiamini, kasumba hii ya
kutarajia ainaya pekee ya kusamehewa na kuvumiliwa kwa kisingizio tuu cha kuwa upo kwenyemapenzi namwenza
wako, hurudisha nyuma maendeleo ya mahusiano yenu kwanimwenzi wako nae
ni binadamu na kumbuka anayo matarajio mengine ya maisha,isitoshe na
yeye anahitaji upendo na
kujaliwa na wewe, hivyo kutarajia
kwakokusamehewa na kuvumiliwa kuna mnyima haki mwenza wako. Hatimaye
kutegema kwakokusamehewa kila wakati, kunamfanya mwenza wako atilie
mashaka upendo wakokwake.
5. Uaminifu = Upendo= Kudumu kwa
mahusiano Pamojana ukweli kuwa mwenza wako anatarajia utakuwa muanifu
kwake, elewa kuwa kuwamwaminifu pekee katika mahusiano yako sio tiketi
ya kudumu kwa mahusiano yenukwakuwa watu wanaingia kwenye mahusiano sio
tuu kwa kuwa wanataka kuwa na mtummoja muaminifu bali wana mahitaji
mengine wanayohitaji. Zungumzana mwenza wako, fanya utafiti wako binafsi
kuhusu mpenzi wako ujue mambomengine anayohitaji toka kwako. Pia
msikilize anapokutaka urekebishe mambokadhaa au ufanye mambo fulani.
Inapendeza pale unapomfanyia mtu
mamboyanayompendezesha kwa kuwa hivyo ndivyo anavyotaka, sio kwakuwa tuu weweunadhani kufanya hivyo kutampendezesha mhusika.