Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia.
Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha sana!
Labda
kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana
yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja
tumepumzika kuizungumzia.
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni
kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi
wengi hufanya makosa.
Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu
ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na
kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati
wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Nalazimika
kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya
makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja
anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni lazima
kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake
na mara nyingi yanaboresha uhusiano.
Kuoga pamoja
Mtakuwa ni
watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala
na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga
ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza
lazima muoge.
Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia
kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi
unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na
huyo wako wa maisha?
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe
ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba,
elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.
Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.
Kusifiana
Hakuna
muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza
kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni
lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.
Msifie kwa
utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na
ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu
yake ujisikie amani ya kupitiliza.
Wapo ambao hawana kabisa kasumba
ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani
wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana
kunanogesha mambo.
Kuelekezana
Kwenye kale kamchezo, wapo
ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la
kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha
wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha
ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na
kubadilika.
Zungumzieni maisha
Huu ni wakati muafaka wa
kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa
zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake.
Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu
kwa ujumla.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa.
Yapo
mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja
kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu